Praise The LORD!
MUNGU ni mwema kila wakati na kila wakati MUNGU ni mwema!
Natumaini unaendelea vizuri na maisha yako ya kila siku.Leo tunaangalia somo linalohusu Imani.
Imani Ni Nini?
Waebrania 11:1
1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Turudie tena kusoma huo mstari hapo juu mpaka ueleweke vizuri.
Ni kuwa na hakika na jambo unalolitarajia.Ni bayana ya mambo ambayo hayajaonekana bado.Maana yakishaonekana kuna haja gani ya kuamini wakati tayari unaona ?
Katika kitabu cha Waebrania 11 tunaona wazee wetu wa zamani waliotutangulia jinsi walivyoenenda kwa Imani.Walienenda katika imani na Mungu alikuwa pamoja nao.
Je,unafahamu mojawapo ya njia ya kumpendeza Mungu ni kuwa na Imani Naye?
Waebrania 11:6
6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Mistari ifuatayo ni vyema tukaisoma na kuitafakari kwa kina ili izame katika mioyo yetu.Inatuonyesha namna Mungu alivyoweka Imani ndani yetu.
Warumi 12:3
........kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.
2Wasethalonike 1:3
........kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.
Warumi 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Ukiisoma vizuri hii mistari hapo juu utagundua kuwa:
1.Mungu humpa kila mmoja wetu kiasi cha Imani.
Kwa nini kila mmoja lazima apewe kiwango fulani cha Imani?
Ni kwa sababu huwezi kuokoka bila kuwa na kiwango fulani cha imani katika Kristo maana Biblia imesema tumeokolewa kwa neema kupitia imani katika Kristo.Bila Mungu kutupa kiasi cha imani kila mmoja wetu,isingewezekana kuokoka kupitia Mwana wake mpendwa Yesu Kristo.
2.Mstari wa pili unatuonyesha kwamba baada ya Mungu kutugawia kila mtu kiasi cha imani,imani hiyo huendelea kukua ndani yetu.Ni rahisi sana mtu kuwa na kiwango kikubwa mno cha imani na Mungu pale mambo yanapokwenda vizuri lakini mambo yanapobadilika na kuwa mazito kiwango cha imani na Mungu hushuka.Ndio maana Mtume Paulo alisema yatupasa kupigana vita vizuri vya imani.Wakati mwingine inabidi kuipigania imani uliyonayo kwa Mungu ili kiwango chako cha kumwamini kisishuke haswa pale mtu unapopitia mazito.
3.Mstari wa tatu unatueleza namna ya kuikuza imani ambayo Mungu ameiweka ndani yetu.Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo.Kusikia Neno la Mungu inamaanisha kusikia Neno La Mungu kama lilivyo katika Biblia,kujisomea mara kwa mara na kulitafakari kwa kina lizame katika moyo.Mungu ni mwaminifu sana.Unapoamini na unavyozidi kujisomea Biblia ndivyo Roho Mtakatifu atakufundisha na kukuelimisha zaidi.Kwa mara ya kwanza kusoma biblia inakuwa kama huelewi mistari lakini kadri unavyoendelea kujisomea na kumshirikisha Mungu ndivyo anavyofungua upeo wako na hatimaye,ufahamu wa mambo ya kiroho unazama taratibu ndani yako.
Kwa leo naishia hapa.Somo hili litaendelea.
Mpaka wakati ujao....
TANZANIA KWA YESU!
No comments:
Post a Comment