Monday, April 21, 2014
ISHI MAISHA YA USHINDI!...YESU YU HAI!
Praise The Lord!Haleluyaaaaa!
Yes,Yesu amefufuka,Yu Hai...Ameshinda kifo na mauti,amemnyang'anya shetani funguo za kuzimu na mauti.
Hii inatuambia nini?Tunapaswa kuishi maisha ya ushindi siku zote kwa sababu aliye ndani yetu yu hai(Marko 16:11)na ni mkuu kuliko huyo wa ulimwengu huu(Yohana 14:30)
Tunaupataje ushindi?
Tusome 1Yohana 5:4-5
'4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?'
Umeona?Tunarudi palepale kwenye somo lililopita linatoka Warumi 10:9-11 ya kwamba
'9Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.'
Kinyume na hapo utaishi maisha ya kushindwa.Utalalamika sana kila siku.Laiti ungejua tu kwamba ukiwa ndani ya Yesu una mamlaka makubwa sana mnoo.Soma Luka 10:19
' 19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.'
Una uwezo wa kuyadunda na kuyafukuza mapepo na ibilisi mwenyewe.Kwa Yesu kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri kwamba yeye ni Bwana(Warumi 14:11).Hivi unafahamu ya kwamba ukiwa ndani ya Yesu umekaa pamoja nae juu katika ulimwengu wa roho?(Waefeso 2:6)
' Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;'
Tuangalie uhalisia:Hivi inakuwaje uwe unakaa pembeni ya raisi kila siku pale ikulu yani upo pembeni yake siku zote na amekupa mamlaka yote halafu usiwe na sauti yoyote.Ukiwa na nafasi kama hiyo kila litokalo mdomoni mwako litafanyiwa kazi.Tena kwa umakini na haraka inavyowezekana.
Sasa ni kwa nini mtu unakubali kuishi maisha ya kushindwa kama upo ndani ya Yesu?(Kama hujampokea Yesu hapo usishangae kwa nini unashindwa)
Bwana Yesu hakuficha,alitamka kabisa katika kitabu cha Yohana 16:33 ya kwamba ulimwenguni mnayo dhiki lakini jipeni moyo,Mimi nimeushinda ulimwengu kwa hiyo ina maana ukikaa ndani ya Kristo,Yeye akawa ndani yako ni LAZIMA utaushinda ulimwengu.
Maisha ya ushindi yanaambatana na kuvaa silaha za Mungu ili tuweze kumpinga yule mwovu...Waefeso 6:10-18 inaeleza vizuri sana habari ya silaha hizi.
Imani inahusika sana katika kufanya mambo yatendeke katika ulimwengu wa roho kabla hayajadhihirika kimwili.Unakumbuka wanafunzi wa Yesu walishindwa kutoa pepo siku moja wakamfuata Yesu faragha wakamuuliza kwa nini walishindwa.Soma Mathayo 17:9-20
Kufunga na Kuomba ni chanzo kingine cha kuwa na nguvu hii ya kutawala kama ambavyo tumepewa.Mathayo 17:21 unaeleza Yesu alivyowajibu kwamba nguvu hii
Unakuta mtu anasema,nitajaribu hiki..mfano labda kuomba kazi mahali fulani,nikikosa basi,sio mpango wa Mungu.Sikiliza nikwambie,kabla hata hujaomba hiyo kazi,mtafute Baba Yako wa Mbinguni.Ongea naye kama unavyoongea na baba yako,kwa heshima zote na uwazi.Maana hata ukimficha Yeye anajua.Mwambie jinsi unavyojisikia kuhusu suala hilo na hiyo kazi unayoitaka.Mungu ni Mungu,Baba,Rafiki na Mwokozi wako.Ni lazima atakujibu tu.Kama kuna hatari mbele yako hutapata msukumo hata wa kuifuatilia hiyo nafasi.Halafu unakuwa na amani tele.Kwa upande wangu mimi nimeshuhudia kwa namna hii mambo kadhaa katika maisha yangu binafsi,ukiacha njia nyingine anazotumia.
Lakini kama anaona kuna usalama mbele napo anakwambia na amani yake itakutawala mno pia.Kama ambavyo ikiwa 'hapana' amani inatawala.Utasikia namna fulani ya kufunikwa na upendo wa Mungu ambao siwezi kuueleza, iwe jibu ni ndiyo au hapana.Jua kitu kimoja,shetani ni bingwa wa kuchakachua lakini suala la ku-pretend tunda la roho especially UPENDO NA AMANI hilo limemshinda kabisaaa.Yani its not him kabisa hawezi kuigiza hicho.Kwa hiyo mara nyingi unapohisi unasukumwa kufanya jambo fulani,angalia pia na amani yako,mtu wako wa ndani anasemaje maana biblia ilishasema tunaongozwa kwa roho,Amani Ya Kristo imeamuaje moyoni mwako?(Wakolosai 3:15a)
Tuangalie uhalisia:Unakuwa na jambo fulani ambalo unataka kulitendea kazi.Mara nyingi mtu humtafuta mtu wake wa karibu sana ambaye anamwamini,halafu anamshirikisha.Inawezekana ikawa mume,mke,rafiki,mzazi n.k.Japokuwa ni sawa,lakini jizoeze kumshirikisha kwanza Mungu mambo yako.Kumbuka Yeye ni Mungu,anajua kila kitu hata ya mbeleni,ambayo unayemshirikisha hayafahamu.Ni Baba,Rafiki,Mzazi yani ameshika nafasi zote za mahusiano mazuri hapa ulimwenguni.Unapozoea kufanya hivyo ndivyo utakavyozidi hata kujifunza namna anavyozungumza nawe.Baadaye inakuwa rahisi sana yani ukiongea naye ukimaliza tu.Ukatulia unamsikia.Mungu huzungumza nasi sana.Ni sisi hatujajifunza kutulia kwa umakini kusikiliza.
Nitakuja kuzungumzia njia ambazo Mungu hutumia kunena nasi huko mbeleni.
Haya mafundisho ni marefu kidogo,Ila Kwa leo naishia hapa...Tukutane tena wakati ujao.
TANZANIA KWA YESU!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment