Monday, July 7, 2014

IMANI (2)


Praise The LORD!...somo letu linaendelea

Imani Bila Matendo Imekufa 
Yakobo 2:14-17

Umeshawahi kumsikia Bwana Yesu akisema maneno kama 'Imani yako imekuponya' (Marko 10:52)kila wakati akimtimizia mtu sawa na alivyoomba?Unapomwomba Mungu jambo ni lazima uishi kimatendo katika imani uliyonayo kwake.Ni kama hivi,mfano una mtoto wako,amekuja amekuomba jambo fulani umsaidie lakini unaona kabisa ana majibu usoni na mashaka kwamba hutamsaidia.Hiyo tu inaweza kukufanya usimsaidie maana yeye ameshaonyesha hakuamini ni tofauti na mtoto huyo huyo akija ana moyo na matumaini yote kwamba utamsaidia.Unajua kutomsaidia huyu itakuwa ngumu sana?Maana kwanza unahofia kumvunja moyo na imani juu yako maana kati ya wote amekuona wewe ndio msaada hakuna mwingine halafu usipomsaidia utauweka moyo wake kwenye hali gani?Huyu mtoto ameonyesha matendo kabisa ya kwamba anakuamini.



Ndivyo ilivyo.Tunaona hata Abraham alitembea katika hali ya kumwamini Mungu mno.Kuanzia alipoambiwa aondoke aende mpaka nchi atakayoambiwa,hadi kumtoa mwana wake wa pekee Isaka.Soma kuanzia kitabu cha Mwanzo 12





Imani Kiasi Cha Punje Ya Haradali Tu,Inang'oa Milima
Matayo 17:20
Punje ya haradali ni ndogo.Lakini ukiwa na imani kiasi hicho tu,unauwezo wa kung'oa milima.Maana yake ni kwamba kiasi hicho hicho kidogo cha imani ulichonacho kina uwezo wa kufanya mambo makubwa yaliyo katika mapenzi ya Mungu,yakatokea.Unachotakiwa ni kukaa katika mstari,kuamini.Hebu angalia punje ya ubuyu,ukiipanda baada ya muda hutaamini kama ni kale kapunje tu ndo ulikokapanda.Vivyo hivyo kwa imani.Ni kama punje ya haradali lakini ina uwezo mkubwa sana wa kubadilisha hali yoyote kwenye maisha.Unatakiwa tu kuiimarisha,isife kama ambavyo punje hiyo ya ubuyu unaimwagilia maji na kuweka mbolea baada ya kuipanda ardhini,ili isife.



Somo hili ni refu kidogo...litaendelea
Mpaka wakati ujao..

TANZANIA KWA YESU!

No comments:

Post a Comment