Saturday, August 2, 2014

Moyo Wa Shukrani Huku Ukimtarajia BWANA



Praise The LORD!

Kila mmoja wetu chini ya jua ameshakuwa na hitaji la namna fulani ambalo alishawahi kutulia na kumwomba Mungu,akajibu.Unapoomba unatakiwa kuamini na kinachofuata tunatakiwa kushukuru.Ukikaa chini ukitafakari vizuri utagundua Mungu alijibu maombi yako mara kadhaa kwenye maisha yako,kama si yote.Je, huwa tunarudi mbele zake kwa ajili ya kumshukuru?

Kuna maombi mengine,ambayo yanahitaji usubiri majibu.Hata unapotuma maombi yoyote,iwe ya kazi au yoyote,itakupasa usubiri majibu.Inaweza ikawa masaa kadhaa,miezi kadhaa au miaka kadhaa.


                          Hold on,HE is going to turn green lights on,sooner than you think.


Kumshukuru Mungu kabla hata jambo halijaonekana dhahiri kwa macho kunaonyesha ni kiasi gani unamwamini kwamba atafanya.Inawezekana ukaona umeishiwa maneno ya kumwambia Bwana ambayo yatawakilisha shukrani zako kwake.Zaburi 138 ni msaada mkubwa katika kumshukuru Mungu ukiwa umtarajia kwamba atafanya.

Zaburi 138

1 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote.
3 Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
4 Ee Bwana, wafalme wote wa dunia watakushukuru, Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.
5 Naam, wataziimba njia za Bwana, Kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.
6 Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.
7 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa kuume utaniokoa.
8 Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.

Anapokuja kujibu maombi yako,ni vyema ukafanya kama ulivyomuahidi,ya kwamba utamshukuru kwa moyo wako wote,utasujudu ukilikabili hekalu lake takatifu..n.k



Mungu ni mwaminifu mno.Unapoomba sawasawa na mapenzi yake hujibu.

Mpaka wakati ujao...
TANZANIA KWA YESU!



No comments:

Post a Comment