Thursday, June 26, 2014

UJASIRI


Ujasiri Ni Nini?
Ni hali ya kutokuwa na hofu kunakoambatana na uthubutu.

Biblia inasema nini kuhusu ujasiri?
Waefeso 3:12
12 Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.

Waebrania 10:19,35
19 Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,
35 Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu.

Kinyume cha ujasiri ni hofu.Ujasiri na Hofu ni roho kamili.Kuna ujasiri kwa upande wa shetani na ujasiri kwa upande wa MUNGU.Unapookoka unafanya mambo ya KiMungu kwa ujasiri.Warumi 5:15 Utumwa wa kishetani huondoka kabisa.



Unapopata uoga wa kufanya mambo mema yanayompendeza Mungu,kemea hiyo hali.Ikatae kwa Jina La Yesu.Hiyo ni roho kamili kutoka kwa Ibilisi.Mfano unaogopa kutoa sadaka,kuchangia huduma za Mungu,kutoa kwa ajili ya wahitaji kama wagonjwa,wajane,yatima,wafungwa kisa unahofu utaishiwa.Hiyo roho kamili kutoka kuzimu ikemee.

Waebrania 4:16
16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Unapata ujasiri wa kuongea na Mungu kuhusiana na jambo lolote lile unapoishi maisha ya kumpendeza.Mungu ni Baba mwenye Upendo.Tuangalie uhalisia,hivi mfano umemkosea mtu jambo fulani,unapata wapi ujasiri wa kumfuata na kuongea naye jambo lolote au hata kuomba msaada kwake kabla hujatengeneza na kumwomba msamaha?
Ndivyo ilivyo kwa Mungu.Mungu hasikii maombi ya wenye dhambi.



Mithali 15:29
29 Bwana yu mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki.
Ukiwa safi una uwezo wa kukaribia kiti chake kwa ujasiri ili kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji,
Kwa maana nyingine,kuna faida ya kuishi maisha safi maana ndiyo yanayotupatia ujasiri wa kupata neema ya Mungu kusikia maombi yetu.



Kwa hiyo ni vizuri kuishi maisha safi,ya kumpendeza Mungu,ambayo yatapelekea kuwa na haki na ujasiri wa kumwomba Mungu na YeYe Mungu anatupa neema inayopelekea kukutana na mahitaji yetu.

Mpaka wakati ujao...

TANZANIA KWA YESU!

No comments:

Post a Comment