Monday, June 9, 2014

Mambo Saba 7 Ya Kufanya Unapopatwa na Uoga - (1)

                                           Acha kustuka kuruka kwa uoga

Praise The Lord!...Halelujaah!

Tunapoona mambo hayaendi kama tulivyotarajia wengi wetu tunaanza kupatwa wasiwasi,kuogopa na kutengeneza taswira kichwani ya mambo mabaya zaidi yanayoweza kutupata kwenye maisha yetu kama hali hiyo ikiendelea.
Cha kushangaza taswira tunazopiga kichwani mara nyingi hazitokei katika uhalisia.Yani tumshukuru Mungu kwa hilo kwa kweli.

                                                   Acha kung'ata kucha kwa uoga

Ni vizuri tukaelewa kwamba kuogopa hakusaidii kubadilisha hali tunazopitia.Kuogopa inatuonyesha jinsi tulivyo dhaifu na tunavyohitaji msaada.Tukiwa kama Wakristo,tunaamini nyakati zetu ziko mikononi mwa Mungu na kwamba Mungu anadhibiti kila hali ya maisha yetu.(Zaburi 31:15Kama tunafahamu hivi,hatuna kitu chochote cha kutufanya tuogope.Nitakupa dondoo saba kutoka kwenye biblia zinazodhibitisha kwamba hatutakiwi kuogopa kabisa katika maisha haya.

(1)Omba
Wafilipi 4:6,7
6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.



Nenda mbele za Mungu,mueleze haja zako na hali zako unazopitia.Mungu ni Baba mwenye Upendo.Atakupa amani kwanza wakati anashughulika na hali uliyonayo.Hakuna haja ya kupatwa wasiwasi,kutolala,kunywa pombe,n.k ili kuondoa mawazo.Hivi vyote havitabadilisha hali unayopitia.Mwambie Mungu.

(2)Mshukuru Mungu
Usikalie kushika bango kwa mambo ambayo huna na huna uwezo wa kuyadhibiti.Angalia vitu ulivyonavyo wewe halafu uangalie kwamba kuna wengine hawana hivyo ulivyonavyo ndio utajua kwamba Mungu bado ni Mwema kwako.Hakuna ubaya wowote kwenda mbele za Mungu ukihoji hali yako na mambo yako alimradi tu usiende ukiwa na hasira mbele za Bwana na kulazimisha kwamba Mungu afanye kwa muda wako na kwa jinsi unavyotaka wewe.Kumbuka YeYe ni Mungu.Anajua kila kitu.Tunatakiwa kwenda mbele zake kwa unyeyekevu,kwa moyo wa shukrani na kumwomba atupe amani ambayo itafungua akili zetu kuelewa mipango yake katika maisha yetu.

(3)Roho Mtakatifu Anakupa Amani
Yohana 14:26,27
26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu

Kazi mojawapo ya Roho Mtakatifu ni Kufariji.Anakusaidia kudhibiti changamoto unazopitia na kukufanya uone wepesi.Sio kwamba hutaona chochote katika hali unayopitia,ni kwamba hutaona ugumu kama uliotakiwa kuuona kama usingekuwa unamtumainia Mungu.

Somo litaendelea ..Unapopatwa na uoga,wasiwasi, nenda katembelee wahitaji kama wagonjwa,maskini,wafungwa na wote waliokwenye wakati mgumu.Wape msaada.Hii itakusaidia na wewe pia tena mno.
 Nakuachia wimbo wa 'What A Wonder Jesus' By Lenny LeBlanc



Mpaka wakati ujao...
TANZANIA KWA YESU!

No comments:

Post a Comment