Praise The LORD!
Wengi wetu tunatamani kumpendeza Mungu.Unapokuwa unampenda mtu fulani ni dhahiri kwamba hupendi kumuudhi na mara nyingi utataka kujua ni vitu gani anafurahishwa navyo ili uvifanye azidi kukufurahia.Kwa Mungu naye ni hivyo hivyo.Kuna mambo kadhaa ambayo unaweza kuyafanya ukamfurahisha sana Mungu.Mimi nimefanikiwa kukuletea mambo kumi na moja(11) kutoka kwenye maandiko,ambayo unaweza kuyafanya ukampendeza Mungu.
1.KUMWAMINI MUNGU- Waebrania 11:6
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
2.KUMSIFU BWANA NA KUMTAFAKARI KWA FURAHA KILA WAKATI-Zaburi 104:33-34
33 Nitamwimbia Bwana maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai; 34 Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Mimi nitamfurahia Bwana.
Biblia ya kiingereza imeandika vizuri badala ya Neno 'na kuwe kutamu kwake' imetumia neno 'pleasing' kama ifuatavyo:
33 I will sing to the LORD all my life; I will sing praise to my God as long as I live.
34 May my meditation be pleasing to Him, as I rejoice in the LORD.
3.KUJITOA KWA MUNGU-Warumi 12:1
1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
4.KUOMBEA DUNIA NA MAMLAKA ZILIZOPO -1 Tim. 2:1-3
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;
Biblia ya kiingereza imetumia neno pleases katika mstari wa tatu badala ya neno 'lakubalika',kama ifuatavyo....
I urge, then, first of all, that requests, prayers, intercession and thanksgiving be made for everyone - for kings and all those in authority, that we may live peaceful and quiet lives in all godliness and holiness. This is good, and pleases God our Saviour.
5.KUZAA MATUNDA NA
6.KUMFAHAMU MUNGU ZAIDI - Wakolosai 1:10
mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;
7. KUZIPA KIPAUMBELE AFYA ZA KIROHO ZA WAKRISTO WENGINE -Warumi 14:15-18
15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.
17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
18 Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.
8. KUWATENDEA SAWA WA NYUMBANI MWAKO -Wakolosai 3:18-21,1Timotheo 5:4
Wakolosai 3:18-21
18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. 19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
20 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.
21 Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
9.UTOAJI -Wafilipi 4:18
18 Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.
10.KUFANYA HAKI KWENYE BIASHARA ZAKO -Mithali 11:1
1 Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. 11.KUENENDA KATIKA MAPENZI YA MUNGU -1Wasethalonike 4:1
1 Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.
No comments:
Post a Comment