Friday, April 25, 2014
TAG Kuadhimisha Miaka 75 Ya Huduma TANZANIA
Makanisa ya TAG nchini yamekusudia kuadhimisha miaka 75 ya uhai nchini Tanzania.Sherehe hizo zinategemewa kuanza kwa ngazi ya kanisa jumapili hii ya tarehe 27.04.2014,ikifuatiwa na ngazi ya Jimbo na mwishowe kuhitimishwa ngazi ya kitaifa mkoani Mbeya katika uwanja wa Sokoine tarehe 13.07.2014.
Kanisa la TAG,ni moja ya makanisa yaliyozaliwa na kukua kwa kasi nchini,huku yakizidi kuongeza mapana yake na kuhudumu mpaka vijijini.Kauli mbiu ya kanisa la TAG ni 'Miaka 10 ya mavuno,Tanzania kwa YESU' lakini kama ujuavyo vijana wameibadilisha na kuitamka 'Miaka 10 ya mavuno,Tutavuna mpaka kieleweke'
Askofu mkuu wa TAG Tanzania,Dk.Barnabas Mtokambali.
Mungu ibariki Afrika,Mungu ibariki Tanzania.
TANZANIA KWA YESU!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment