Natamani kesho ifike yani natamani kweli.Kwa matayarisho ambayo nimeyaona,siku ya kesho itafana mno!Leo siku nzima toka saa nne asuhuhi nilikuwa kanisani kwetu Kimara TAG.Nikiwa kama mwana-team wa sifa na kuabudu,tulikuwa masaa kadhaa ya kufanya mazoezi ya nguvu sana kwa ajili ya siku muhimu ya kuadhimisha miaka 75 ya huduma hai ya makanisa ya TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD(T.A.G)
Kila mmoja wetu yupo 'excited' na shughuli hii muhimu.Mbali na kuadhimisha miaka 75 pia siku hiyo ya kesho ni siku ya Sifa na Kuabudu kanisani kwetu.Woow I love this!
Nimeshatayarisha familia yangu kabisa wanajua tunahamia kanisani kesho.Tunaondoka saa moja asubuhi na tunaenda kumwabudu,kumwimbia,kumsifu Bwana mpaka saa moja usiku.Period.Kuna vyakula huku huku kanisani tutakula,na wale wanangu wadogo nitawabebea vigodoro vyao vile vidogo watalala wakichoka.Ni mwendo wa kumwabudu Bwana.Ikumbuke siku ya sabato na uitakase.Nitawakazisha buti kwa Bwana mpaka kieleweke.Hii dunia ya sasa sio ya kuichekea.Ni mwendo mdundo na Mungu.
Mazoezi yalikuwa mazuri mno!.Tumemaliza saa moja usiku.Tumekula pamoja na kupata muda wa kubadilishana mawili matatu.Nikaona si vibaya nikakupa hapa na pale ya yale yaliyotukia.
**BONYEZA PICHA KUPATA UKUBWA KAMILI**
Kanisa likipambwa na mwana timu ya sifa na kuabudu
Kazi ya kufunga vyombo pamoja na wana timu yetu
Mwenyekiti wa timu ya sifa na kuabudu akipumzika kidogo
Testing microphone...
Ngoma zikiwekwa sawa
Balancing sauti za kila chombo
Tukisubiri wenzetu wakati vyombo vinafungwa
Nyimbo zikiwekwa sawa
Mazoezi yakianza...
Ilipigwa strings hapa,safi sana!
Bass guitar likingurumishwa...hapakutosha
Kinanda no.2 kikipigwa kwa mvuto wa pekee..
Drums zikipigwa kwa ustadi wa hali ya juu..
Solo guitar lilipigwa kwa umaridadi kabisa
Mazoezi ya kuimba yakiendelea..
Zoezi kali toka saa nne asubuhi hadi moja usiku
Vyombo vikipigwa kwa ustadi wa hali ya juu
Kama baba,kama mtoto.Kuza kipaji cha mwanao mapema
Dada akiongoza nyimbo za sifa...
Yakaletwa mavuvuzela kwa ajili ya shughuli ya kesho
Yakijaribishwa kama yako vizuri..
Kila mmoja alichukua lake kujaribisha..yapo saizi zote tena mengi sana
Huyu mtoto kanipendaje?Kati ya wote akanichagua mimi kaniletea bisi zake..
Nilitaka niwawekee video ndogo ya nyimbo za mazoezi lakini antivirus yangu inadhani kila kitu ni kirusi basi hata converter niki-install inaikatalia;halafu sasa hivi ni saa nne usiku na kukikucha ndio siku ya shughuli yenyewe natakiwa niwe 'active' siku nzima non stop mpaka saa moja usiku ndo nitakuwa huru kurudi nyumbani hivyo yanipasa nipumzike mapema.
Nitawawekea yatakayojiri kesho jumatatu.
MIAKA KUMI YA MAVUNO,TANZANIA KWA YESU!(Kauli mbiu ya TAG wote)
MIAKA KUMI YA MAVUNO,TUTAVUNA NA YESU MPAKA KIELEWEKE!( vijana wa TAG wameichakachua)
No comments:
Post a Comment