Mungu ni Mtakatifu.Sana.Nampenda sana sana Mungu kwa sababu YeYe ni Halisi na nimemuona mno katika maisha yangu.Upendo wake juu yangu ni mkuu sana.Hauelezeki.
Niliamka alfajiri nikaanza kupiga stori nae.Sio kila wakati ukienda kwake uwe unataka hiki mara kile.Kuna wakati wa kuongea,kucheka,kushauriana na kisha kumshukuru kwa uwepo wake mahali hapo.Unaweza ukaona kama naongea kiyunani flani hivi, 'its funny' lakini kwa kweli nikiwa kwenye mazingira yale na nikausikia uwepo wake yani sitaki sitaki chochote kiniondoe.Na ndio maana huwa nafanya hivi usiku wa manane ili watoto wasije wakanigongea kunisumbua.
Unajua hata kwa hali ya kibinadamu jamani,kama una watoto,mmoja akawa kila mara anakuja kwako anaanza kukueleza uzuri wako na ku-appreciate yote uliyomfanyia,kukwambia kwamba atakuwa nawe daima,atakuheshimu na anakupenda mno.Kila mara anafanya hivyo.Siku akija na shida utamsikiliza haraka mno na kumsaidia tofauti na mtoto ambaye haonekani hata siku moja kuja kuongea nawe,hana muda,wakati mwingine unamwita anauchuna haitiki,siku hata akija na shida utamsaidia tu kwa sababu ni mwanao lakini kwa kujivuta.Yale mahusiano hayapo,kitu ambacho ni muhimu sana.Ndivyo ilivyo.Hata 'Baba' ana hisia.Anataka mahusiano mazuri na watoto wake.Wengi wanadhani Baba ameshika kiboko tuu saa zote yupo tayari kuhukumu,la hasha.Ni baba mwenye upendo mwingi lakini pia akikuadhibu anafanya kwa upendo ili ujifunze sio uangamie.
Nimeamka nina wimbo huu unaimba moyoni umeendelea kuimba mpaka sasa.
Ni vizuri ukamwambia Mungu jinsi alivyo Mtakatifu,jinsi unavyoheshimu nafasi aliyokupa kumwabudu na kusimama mbele zake kumtumikia,jinsi alivyo ni sababu tosha ya sisi kuamka alfajiri na kumwimbia n.k.Haya ni maneno yaliyo kwenye wimbo huu niliomka nao wa mwanadada Juanita Bynum.
Holy By Juanita Bynum...Karibu.
No comments:
Post a Comment