Monday, April 28, 2014

Maadhimisho Ya Miaka 75 Ya TAG YAFANA!



Tunamshukuru sana Mungu maana yale maadhimisho tuliyoyasubiri kwa hamu kubwa,ya miaka 75 ya TAG yamefana sana.Kanisani kwetu kulijaa shamrashamra nyingi toka asubuhi ni nyuso za furaha,haleluya,zilitawala.Kanisa letu la Kimara lipo jimbo la Mashariki-Kaskazini.Watu walikuwa wachangamfu na wenye nguvu za kutosha,si watoto,vijana,wamama,wababa,watu wazima wote tulikuwa level ya ujana.Kila mtu alikuwa anaruka,kuimba na kucheza kwa furaha mbele za Mungu.

Kulikuwa na t-shirt rasmi za aina mbili.Rangi ya zambarau na nyingine za rangi ya kahawia.Mbali na hayo kila sekta ilikuwa na sare rasmi za kujitambulisha kama wewe ni baba,mama,mtoto,n.k mfano wababa walivaa suti nyeusi,wamama walikuwa na vitenge vyao,vijana wa CAs walikuwa na sky blue,Evershine kwaya black yenye batiki ya pink,watoto na walimu wao na wachungaji walivaa t-shirts n.k

Nilijitahidi kidogo kukusanya matukio,japo changamoto ilikuwa ni kuzipata vizuri picha maana 'movements' zilikuwa nyingi kidogo...

                                         Chama Cha Wanaume(CMF) wakiimba..
                                         Kwaya ya watoto ikafuatia...
                                         Kwaya ya wamama..
                                         Wamama wakiendelea kutumbuiza...
Sisi ni watoto tuliokuwepo kipindi kile miaka ya 1980,tuliimba nyimbo zetu za utotoni tulizofundishwa,tukasema mistari ya kukariri kama tulivyofanya huko nyuma miaka ya 1980 tukiwa wadogo

                                         Wa tatu kutoka kushoto ndiye aliyekuwa mwalimu wetu wa utotoni.

Anaitwa Raymond.Huyu mtoto ana uelewa wa aina yake.Anasema mistari ya Biblia kwa kichwa kama ilivyoandikwa bila kuisoma.Ameshindanishwa kote akashinda na amechaguliwa kwenda Mbeya kwenye hitimisho la miaka 75 ya TAG kitaifa.Mungu akubariki Raymond.Hata shuleni nasikia yuko vizuri mnoo.

                                          Watu wakifuatilia kwa makini...
                                         Mtoto Raymond aliwakosha sana watu..yupo vizuri.
Mchungaji Mkuu wa Watoto,Mch.Sarafina Kashaga akimzungumzia mtoto Raymond.Nyuma ni mzee wa wetu wa Kanisa wa toka enzi za mwanzo,Mzee Mwihava.

                                         Kwaya kutoka temboni wakitumbuiza kwa wimbo..
                                          Evershine Kwaya wakiingia kwa furaha
                                          Waumini wa Kimara TAG tumeongezeka,Asante Yesu
                                         Mama mtu akimshukuru Mungu kwa kujifungua salama..
                                          Mtoto akiombewa...alitulia kimyaa.
                                          Shetani usije ukaota ndoto zako juu ya mtoto huyu...tumeshakuonya mapema.
                                         Mabalozi wa Yesu(kwaya ya vijana)ikiingia kwa mbwembwe
                                         Kutoa sadaka...
                                         Walipiga kwata ya nguvu...
                                         Sadaka zikiombewa...
                                        

                                         Uliimbwa wimbo wa zamani 'Siku ni hii Bwana amefanya'
              Kuadhimisha,tuliachia hewani puto moja baada ya lingine.Kila puto liliandikwa miaka 75 ya TAG

                                         Watu wakilifuatilia kwa makini puto lililoachiwa na mchungaji..
                                         Puto lileee linaondoka zake taaratibuu
                                          Mkuu wa Kituo cha Polisi Kimara Afande Mfaume Msuya akiachia puto lake..
                                          Puto la afande likijiondokea zake...
                                          Picha za haraka haraka wakati tunakaribia kula...

                                         Kodak moments zikiendelea....
                                         Msosi time...
                                          Chakula kilikuwa kitamu mnoo
                                         Wako hoi..wameimba,wamecheza,wamekula,wamekunywa,wanawaza kitanda..
                                         Wamechangamka baada ya kufika nyumbani...


                                         

Zikaanzishwa rehersal za nyimbo zilizoimbwa mchana...huyu mwenzetu katikati kila likija suala la kupiga picha anapataga usingizi....



                                                 

ohooo ukiona 'curiosity faces' zimeanza zikiambatana na kunyata, ujue 'device' uliyoshika haina usalama tena...


Baada ya hapo nilirudi kanisani kwa ibada ya sifa na kuabudu.Kamera ilichemka zile shughuli za siku nzima zilimaliza betri,Hivyo sikufanikiwa kupiga picha za sifa na kuabudu.
.. Itabidi aidha ninunue betri nyingine orijino kama zipo,au kamera nyingine ya standby...Baba yangu wa mbinguni anajua ninahitaji haya.Ngoja mimi niutafute kwanza Ufalme Wa Mbinguni na Haki yake,haya mengine yote atanizidishia.Mathayo 6:33

MIAKA 10 YA MAVUNO,TANZANIA KWA YESU!..TUTAVUNA MPAKA KIELEWEKE!

1 comment:

  1. Niiice...hongereni sana.Namwomba Mungu azidi kuliimarisha kanisa lake..!

    ReplyDelete