Tuesday, October 4, 2016

BLESS,PRAISE,MAGNIFY,BOAST,EXALT - Psalm 34:1-8




I will bless the Lord at all times;
His praise shall continually be in my mouth.

My soul makes its boast in the Lord;
The humble and downtrodden will hear it and rejoice.

[a]magnify the Lord with me,
And let us lift up His name together.

I sought the Lord [on the authority of His word], and He answered me,
And delivered me from all my fears.

They looked to Him and were radiant;
Their faces will never blush in shame or confusion.

This poor man cried, and the Lord heard him
And saved him from all his troubles.

The [b]angel of the Lord encamps around those who fear Him [with awe-inspired reverence and worship Him with obedience],
And He rescues [each of] them.

O taste and see that the Lord [our God] is good;
How blessed [fortunate, prosperous, and favored by God] is the man who takes refuge in Him.

Friday, August 15, 2014

Namna Kumi na moja(11) Za Kumpendeza Mungu


Praise The LORD!

Wengi wetu tunatamani kumpendeza Mungu.Unapokuwa unampenda mtu fulani ni dhahiri kwamba hupendi kumuudhi na mara nyingi utataka kujua ni vitu gani anafurahishwa navyo ili uvifanye azidi kukufurahia.Kwa Mungu naye ni hivyo hivyo.Kuna mambo kadhaa ambayo unaweza kuyafanya ukamfurahisha sana Mungu.Mimi nimefanikiwa kukuletea mambo kumi na moja(11) kutoka kwenye maandiko,ambayo unaweza kuyafanya ukampendeza Mungu.

1.KUMWAMINI MUNGU- Waebrania 11:6
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.



2.KUMSIFU BWANA NA KUMTAFAKARI KWA FURAHA KILA WAKATI-Zaburi 104:33-34
33 Nitamwimbia Bwana maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai;
34 Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Mimi nitamfurahia Bwana.
Biblia ya kiingereza imeandika vizuri badala ya Neno 'na kuwe kutamu kwake' imetumia neno 'pleasing' kama ifuatavyo:
33 I will sing to the LORD all my life; I will sing praise to my God as long as I live.
34 May my meditation be pleasing to Him, as I rejoice in the LORD.

3.KUJITOA KWA MUNGU-Warumi 12:1
1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

4.KUOMBEA DUNIA NA MAMLAKA ZILIZOPO -1 Tim. 2:1-3

1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;

 Biblia ya kiingereza imetumia neno pleases katika mstari wa tatu badala ya neno 'lakubalika',kama ifuatavyo....

I urge, then, first of all, that requests, prayers, intercession and thanksgiving be made for everyone - for kings and all those in authority, that we may live peaceful and quiet lives in all godliness and holiness. This is good, and pleases God our Saviour.



5.KUZAA MATUNDA NA 
6.KUMFAHAMU MUNGU ZAIDI - Wakolosai 1:10
mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;

7. KUZIPA KIPAUMBELE AFYA ZA KIROHO ZA WAKRISTO WENGINE -Warumi 14:15-18
15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.
17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
18 Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.



8. KUWATENDEA SAWA WA NYUMBANI MWAKO -Wakolosai 3:18-21,1Timotheo 5:4
Wakolosai 3:18-21
18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.
19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
20 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.
21 Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

9.UTOAJI -Wafilipi 4:18
18 Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.

10.KUFANYA HAKI KWENYE BIASHARA ZAKO -Mithali 11:1
1 Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.

11.KUENENDA KATIKA MAPENZI YA MUNGU -1Wasethalonike 4:1
1 Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.




Nakuachia wimbo huu Umpendeze nao Bwana, wa Lord I lift you name on High



Mpaka wakati ujao,
TANZANIA KWA YESU!

Tuesday, August 12, 2014

Today's Prayer...




Jipe Moyo Mkuu,Jikabidhi Kwa BWANA.

ZABURI 27

1 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
2 Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
3 Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.
4 Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.
5 Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.
6 Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi Bwana.
7 Ee Bwana, usikie, kwa sauti yangu ninalia, Unifadhili, unijibu.
8 Uliposema, Nitafuteni uso wangu, Moyo wangu umekuambia, Bwana, uso wako nitautafuta.
9 Usinifiche uso wako, Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira. Umekuwa msaada wangu, usinitupe, Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.
10 Baba yangu na mama yangu wameniacha, Bali Bwana atanikaribisha kwake.
11 Ee Bwana, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea;
12 Usinitie katika nia ya watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo wameniondokea, Nao watoao jeuri kama pumzi.
13 Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana Katika nchi ya walio hai.
14 Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.



Usisahau kuwaombea na wengine 


Mpaka wakati ujao,

TANZANIA KWA YESU!

Wednesday, August 6, 2014

Imani Yako Imekuponya



Praise The Lord!

Unapokuwa ndani ya Yesu,unapaswa kujua haki zako.Kuzifahamu haki zako vyema,ni lazima usome Biblia,utafakari maandiko.Roho Mtakatifu atakukukumbusha na utaweza kutumia maandiko hayo pindi unapopatwa na hali fulani.

Mungu wetu,ni Mungu asiyeshindwa na jambo lolote.Anafanya kila kitu,na ni Mungu anayeponya.Ngoja nikupe ushuhuda kidogo...



Kati ya wanangu Mungu alionibarikia,nina mapacha.Sasa huyu pacha mdogo au kwa lugha nyingine dotto,alikuwa mzima tu lakini juzi jioni,alikuwa 'restless'.Analala kidogo,anaamka akiwa analia,na mara nyingine anashika kichwa huku analia.Hajajua kujielezea sana hivyo nilikuwa kwenye wakati mgumu kidogo kujua nini kinamsumbua.Kufika mida ya saa tatu usiku,alikuwa na dalili za joto,kula hajisikii yani hata vile vyakula anavyopenda sana nikimpa anavisogezea mbali.Nikajua kuna tatizo.Iwe malaria,iwe UTI, au nini lakini kuna tatizo.Nikamwambia Mungu pesa ulizonibarikia umeziwekea ulinzi tayari na kwamba utamkemea yule alaye isivyo halali maana mimi ni mtoto wako na ninatoa fungu la 10 sadaka na zaka.

Malaki 3:10-11 inasema
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.

(Hivi unafahamu kuwa kutokutoa fungu la 10,sadaka na zaka kunafanya kinyume cha hayo yaliyoandikwa hapo?Laana,mikosi,mabalaa yanapata milango hapo.Hili somo nitakuja kulifundisha muda si mrefu.It's very serious.It affects your spiritual and physical life indeed)



Nikamchukua mwanangu nikaingia naye chumbani,nikafungua Biblia,hatukwenda mbali tukaanza na Kumbukumbu la Torati 28:7
7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Nikamshikisha kwa mikono biblia huku nikimtakia maneno ya mstari huo.Baada ya hapo tukahamia kwenye Isaya 53:5
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.


Nikaanza kumwomba Mungu huku nikikemea kila hila za yule adui na kuachilia uzima na afya njema.Nilipomaliza,na yeye akajibu Amen.
Usiku wakati amelala nikaenda kumwangalia,nikakuta jasho linamtiririka sana,nikamfuta,nikamshukuru Mungu kwa uponyaji unaoendelea nikarudi kulala.Asubuhi alivyoamka tu akanifuata na kikombe akaniambia anataka maji ya kunywa.Nikampa.Baada ya hapo alikuwa anakula kila kitu,anakimbia,anacheza, kachangamka mnoo.Nilimshukuru Mungu kwa uponyaji huo.Mpaka sasa navyoandika hapa ni mzima kabisa.Yes,Mungu wetu ana nguvu,ni mkuu,hakuna neno gumu kwake.
,
Bwana Yesu alipokuwa anaponya watu,aliangalia pia kama wanaamini anaweza kuponya.
Soma Luka 17:19, Marko 10:52, Luka 8:48
Wale wote waliokuja kwake wakiwa wanaamini bila shaka kwamba atawaponya,walipona hapo hapo.
Licha ya mambo niliyoeleza hapo juu,imani yako pia inahusika sana.Kama unamwendea Mungu ukiwa una mashaka,umelikuza tatizo na kuliona ni kubwa kuliko Mungu wetu,hutaweza kupokea.Fanya upande wako ili na Mungu afanye upande wake.Mkabidhi Bwana Yesu maisha yako kwanza,muamini jumla,halafu ishi sawa sawa na Neno Lake.



Mpaka wakati ujao..
TANZANIA KWA YESU!

Saturday, August 2, 2014

Moyo Wa Shukrani Huku Ukimtarajia BWANA



Praise The LORD!

Kila mmoja wetu chini ya jua ameshakuwa na hitaji la namna fulani ambalo alishawahi kutulia na kumwomba Mungu,akajibu.Unapoomba unatakiwa kuamini na kinachofuata tunatakiwa kushukuru.Ukikaa chini ukitafakari vizuri utagundua Mungu alijibu maombi yako mara kadhaa kwenye maisha yako,kama si yote.Je, huwa tunarudi mbele zake kwa ajili ya kumshukuru?

Kuna maombi mengine,ambayo yanahitaji usubiri majibu.Hata unapotuma maombi yoyote,iwe ya kazi au yoyote,itakupasa usubiri majibu.Inaweza ikawa masaa kadhaa,miezi kadhaa au miaka kadhaa.


                          Hold on,HE is going to turn green lights on,sooner than you think.


Kumshukuru Mungu kabla hata jambo halijaonekana dhahiri kwa macho kunaonyesha ni kiasi gani unamwamini kwamba atafanya.Inawezekana ukaona umeishiwa maneno ya kumwambia Bwana ambayo yatawakilisha shukrani zako kwake.Zaburi 138 ni msaada mkubwa katika kumshukuru Mungu ukiwa umtarajia kwamba atafanya.

Zaburi 138

1 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote.
3 Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
4 Ee Bwana, wafalme wote wa dunia watakushukuru, Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.
5 Naam, wataziimba njia za Bwana, Kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.
6 Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.
7 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa kuume utaniokoa.
8 Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.

Anapokuja kujibu maombi yako,ni vyema ukafanya kama ulivyomuahidi,ya kwamba utamshukuru kwa moyo wako wote,utasujudu ukilikabili hekalu lake takatifu..n.k



Mungu ni mwaminifu mno.Unapoomba sawasawa na mapenzi yake hujibu.

Mpaka wakati ujao...
TANZANIA KWA YESU!



Tuesday, July 29, 2014

Mafanikio Ya Ki-MUNGU





Praise The LORD!
Mungu yu mwema kila wakati....

Leo tuongee kidogo kuhusu mafanikio.Kuna mafanikio yanayotoka kwa Mungu na yale yatokayo kwa yule mwovu,ibilisi.Mafanikio yanayotoka kwa Mungu huwa yanadumu,maana yana ulinzi wa Mungu ndani yake,hayana masharti.Nira ya Mungu ni laini Mathayo 11:29-30 tunaona Bwana Yesu anawaasa ya kuwa wajifunze kutoka kwake,maana yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo na kwamba watapata raha nafsini mwao,maana nira yake ni laini,na mzigo wake ni mwepesi. Mungu ni BaBa mwenye upendo.Akikubariki anafanya hivyo kwa moyo wake wote.Anakubariki baraka za rohoni mpaka za mwilini pia,anakupa amani wakati wote.

Lakini haya yote hayaji hivi hivi tu,kuna gharama za kulipa lakini gharama hizi ni nyepesi sana.Sio kama za shetani,ambazo ni ngumu sana,nzito,zinazogharimu maisha ya wapendwa wako kila mara,halafu mafanikio yenyewe hayadumu,tena yana masharti yasiyofaa, ya kudhalilisha.

Katika kitabu cha Yoshua 1:7-9 BWANA alikuwa anaongea na Yoshua baada ya Musa kufa akamwambia,

7 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.

8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. 

9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.



Mambo makuu matatu(3) Tunayotakiwa Kufanya

1) Tunakiwa kuwa hodari na wenye ushujaa mwingi.
Ina maana kuelekea kwenye mafanikio utakutana na vikwazo vingine vinakaribia kukatisha tamaa kabisa maana kumbuka kwanza shetani hapendi uwe levo nyinigine ya juu.

Mungu alimsisitiza Yoshua ya kwamba awe hodari na mwenye ushujaa mwingi.Kwa kifupi Mungu hapendi mtu uwe na tabia ya woga maana kwanza woga hautokani naye.2 Timotheo 1:7 inasema 
'Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi'.  

2)Uangalie na kutenda sawasawa na maandiko yanavyosema,usigeuke kulia wala kushoto.Kwa maana nyingine usipindishe chochote.Hapa sasa ndio tuulizane.Tunasoma maandiko kila siku?Tunayaelewa vizuri?Tunayatafakari mchana na usiku kuyazamisha kwa kina kwenye mioyo yetu?




Hivi unafahamu maandiko ndiyo mwongozo wote?Kuna majibu ya mambo yote chini ya jua kupitia maandiko ambalo ni Neno la Mungu lililo hai.Ndio maana mtunga Zaburi aliona hili na akasema wazi katika Zaburi 119:105  ya kwamba 
105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.

Usiposoma maandiko unajuaje haki zako?Unajuaje namna ya kumshinda shetani?Unajuaje mambo unayotakiwa kufanya na usiyotakiwa kufanya?Mungu anazungumzaje nawe?japo zipo njia nyingi ambazo huwa anatumia lakini hii huitumia sana maana ni lazima athibitishe kila asemalo kupitia Neno lake au maandiko.Kwa kifupi kama hatusomi Biblia,tuanze.Kuna majibu ya maswali yote chini ya jua.Roho Mtakatifu ni mwalimu mzuri sana.Atakufundisha,utaelewa.Maana Biblia si kitabu mtu akisoma anakielewa kirahisi.Lakini ukishampokea Bwana Yesu na Roho Wa Mungu akawa ndani yako,anakufundisha unaelewa vizuri sana.



3)Uwepo wa Mungu kwenye maisha yako.Tunaona kwenye mstari wa 9 hapo juu Mungu alimhakikishia Yoshua kwamba yupo pamoja nae kila aendako.Na Mungu akiwa upande wako ni nani anaweza kuwa kinyume chako?

Sasa swali kwetu,umeshamkiri Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako?Maana ukishamkubali tu,anatembea pamoja nawe kila uendako na ndio mwanzo wa kufanikiwa maana YeYe,Mungu Baba na Roho Mtakatifu watafanya makazi ndani yako na watakuongoza na kila unapotii na kufanya vile Roho Mtakatifu anavyokuamuru,utafanikiwa.

Barikiwa sana.
Mpaka wakati ujao,
TANZANIA KWA YESU!

Tuesday, July 22, 2014

Je,Unafahamu Vipaji Ndani Ya Wanao?




Praise The Lord!

Watoto ni baraka njema mno kutoka kwa Mungu.Nikiwa kama mzazi niliyebarikiwa watoto wazuri watatu,mmoja wa miaka mitano na mapacha wa miaka miwili,nimeanza kuwa-expose kwenye mazingira tofauti ili nione nini kila mmoja anapenda.

Ninapoanza kumsifu Mungu kwa kupiga kinanda huku naimba,wote wanakuja haraka sana na wanaimba na mimi huku wakionyesha kila dalili kwamba wanatamani kupiga chombo hicho nami.Nikiwa na-design nguo na kushona,yule mkubwa huwa anaonyesha 'interest' sana.Kwa hiyo najua nikimuweka vizuri naweza nikapata designer mzuri sana wa nguo hapo,licha ya kuwa mpigaji mzuri wa kinanda.

Bado ninaendelea kufanya utafiti wa kuwaweka mazingira tofauti tofauti ili nione nini kingine ambacho kila mmoja atakuwa anapenda,kama si wote.Ili kufanikisha hili inahitaji mtu uwe 'multi-purpose'.Uwe na vipaji vingi na uwe unavitumia wakiwepo.Si jambo rahisi sana,ila 2Wakorintho 9:6 inasema Apandaye haba atavuna haba.... Na lingine Wagalatia 6:7-8 'Msidanganyike mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu ndicho atakachovuna maana yeye apandaye .......

Huyu mtoto pichani juu na kwenye video chini, anaitwa Jotta.Ametokea Brazil.Amenikosha moyo sana.Nina uhakika hata Mungu akimwona anamfurahia maana ni chombo chake kizuri sana cha kusifu na kuabudu.Ameimba wimbo ule wa Agnus Dei,Halelujah,wa Michael Smith.

omg! anaimba vizuri mnooo....hebu msikilize....






Hiki ndio ninachozungumzia. Tunapanda nini kwa watoto wetu? Tunataka mtu/watu wa aina gani kwenye familia,jamii na taifa baada ya miaka kadhaa? Mungu atusaidie tuwakuze vyema. Mpaka wakati ujao... TANZANIA KWA YESU!

Thursday, July 17, 2014

UAMINIFU WA MUNGU NI MKUU





Kumbukumbu 7:9

9 Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu;

Praise The LORD!
Mungu wetu ni mwaminifu mnoo!Haijalishi umemwomba nini ali mradi iwe sawasawa na mapenzi yake na uwe unamcha na kumpenda,atafanya.Unapomwomba,muamini.Muachie.
Isaya 41:21 amesema "Haya,leteni maneno yenu,asema BWANA;toeni hoja zenu zenye nguvu,asema mfalme wa Yakobo'.



Ukiona ka-muda kanakwenda,mkumbushe.Maana amesema hata kwenye neno lake katika Isaya 43:26 'Unikumbushe,na tuhojiane;eleza mambo yako,upate kupewa haki yako.'

Nina ushuhuda wa haraka ambao umenitokea leo hii hii juu ya jambo hili.Wiki mbili zilizopita kuna jambo fulani ambalo nilikuwa ninalihitaji mno mno kulifanya na ufumbuzi wake usipite hizi wiki mbili.Nilipokuwa naomba usiku nikamshirikisha Mungu.Wakati naendelea kuomba nikasikia sauti ya utulivu sana ikiniambia mshirikishe 'fulani' hilo jambo.Pale pale nikajua Mungu anataka kumtumia huyo mtu kunisaidia kulipatia ufumbuzi.Nikamwomba palepale Mungu kibali kwamba nitakapoenda kumshirikisha huyo mtu,alipokee,na anipatie ufumbuzi.Hiyo ilikuwa ni wiki mbili zilizopita.

Kesho yake nikampigia simu yule mtu,tukaongea vizuri akaniambia jioni ya siku inayofuata tuonane.Siku iliyofuatia kweli nikaenda.Nikamshirikisha kila kitu lakini cha kushangaza nilisahau kumwambia deadline.Akaniambia nimuachie alifanyie kazi.Tukaachana.Kwa kifupi alikuwa ameelewa.Wiki ikapita,huku naona wiki moja tu imebaki linatakiwa ufumbuzi.Nikampigia simu yule mtu kumkumbusha,akanipa jibu la nusu nusu au fifty fifty.Ni kama atanisaidia lakini inavyoonekana itakuwa nje ya muda ambao jambo hili linahitaji.Kwa maana nyingine hata akinisaidia muda huo kama ni zaidi ya wiki moja ambayo ndiyo imebaki,huo msaada hautakuwa na maana tena kwangu maana muda utakuwa umepita.Nikawa mpole.



Mwisho wa hiyo siku ulikuwa ni kesho.Toka jana jioni nilikuwa katika hali ya upole sana.Shetani naye hakucheza mbali  nilikuwa nasikia enhe?! za hapa na pale.'Enhe?!kiko wapi?Yuko wapi Mungu?au ndo ushaharibu mahali.Mbona hajibu.Utakuwa umeharibu mbona hajibu?Nilimwambia shetani hata uongee vipi hainibadilishi kutokuwa mtoto wa Mungu na nikamwambia Mungu hata kama halitafanyika utabaki kuwa Mungu,hautabadilika,wala mtazamo wangu kwako hautabadilika.Hayo ndiyo maneno niliyokuwa nayasema kila nikikumbuka kwamba muda unakwisha halafu kimyaa!

Leo asubuhi nikaamka nikamshukuru Mungu kwa kifupi tu,nikasema maneno yale yale tena utabaki kuwa Mungu kwangu na nitakuabudu siku zote mimi na familia yangu.Ikafika kama saa tano asubuhi,nikakaa chini mahali nikamwambia Mungu nakutegemea,naomba unisaidie.Nikaondoka kwenda na mambo yangu mengine.Nilipofika napokwenda nilipotulia chini nikaona missed call ya yule mtu ilipigwa kumbe saa sita kasoro nadhani nikiwa naendesha  gari, simu ipo kwenye pochi sikusikia.Nikampigia yule mtu,akaniambia nimekutafuta kwenye simu sana,nimeshalipatia ufumbuzi jambo lako uje leo hii hii!Yani alikuwa anaongea kwa msisitizo kama vile nisikose.Haleluya!Mimi nimeshangaa kwa sababu yule mtu hakuwa anajua 'deadline' ya hilo jambo kuwa ni kesho.
Huyu ndiye MUNGU tunayemwabudu aisee.Nina shuhuda nyingi mno mno kwenye maisha yangu katika nyakati tofauti ambazo Mungu amekuwa akinitendea mambo makuu.Tutakuwa tunashirikishana.



Zaburi 91:4
4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

Kwa leo naishia hapa.Mungu akubariki.


Friday, July 11, 2014

Ongea Na Nafsi Yako,Imshukuru MUNGU kila siku




The LORD reigns!
Tunapaswa kumshukuru MUNGU kila siku kwa kila jambo.Tunapoamka salama asubuhi ni jambo la kushukuru vile vile kabla ya kulala yatupasa kushukuru.Ikiwezekana muda wowote mzuri unaoupata,ongea na Mungu.YeYe yupo kila mahali wakati wote.Anakuona vizuri anakusikia,anajua yote hata ambayo yamejificha kwenye roho yako ambayo huenda huyafahamu.Tumaini lote liwe kwa Mungu maana Mungu akiwa upande wetu hakuna anayeweza kuwa kinyume chetu.

Wanadamu tumeumbwa tuna mwili,nafsi na roho.Mwili unaonekana ndio maana mtu anaweza kusema nimemuona fulani pale akinunua vitu dukani,nafsi  haionekani kwa macho ila inawasilisha ujumbe wake kupitia mwili.Roho ya mwanadamu nayo haionekani kwa macho ila ndo kila kitu.Inatunza kila jambo la mwanadamu.



Nafsi inasikia vizuri sana unapoongea nayo,unapoiamuru jambo fulani.Mfalme Daudi kwa kulijua hili,alikuwa anaongea na nafsi yake mara kwa mara huku akimwambia Mungu ni kiasi gani anamtegemea na kumtazamia katika maisha yake.

Wakati mwingine unakuwa umechoka lakini roho yako inataka kumsifu Mungu kwa matendo yake katika maisha yako.Hata kumsifu Mungu,kuomba unasikia huwezi.Umechoka.Unaweza ukachukua Biblia yako ukafungua Zaburi.Hiki ni kitabu kimejaa maombi,sifa na mengineyo mengi yanayoweza kueleza unavyojisikia,haja zako n.k mbele za Mungu kwa kina.Mojawapo ya zaburi nayopenda kuisoma
Zaburi 145


Ukuu na Wema wa Mungu 

1Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza,
Nitalihimidi jina lako milele na milele.
2Kila siku nitakuhimidi,
Nitalisifu jina lako milele na milele.
3BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,
Wala ukuu wake hautambulikani.
4Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako,
Kitayatangaza matendo yako makuu.
5Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako,
Na matendo yako yote ya ajabu.
6Watu watayataja matendo yako ya kutisha,
Nami nitausimulia ukuu wako.
7Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu.
Wataiimba haki yako.
8 BWANA ana fadhili, ni mwingi wa huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
9 BWANA ni mwema kwa watu wote,
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.
10 Ee BWANA, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
11Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako.
12Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
14BWANA huwategemeza wote waangukao,
Huwainua wote walioinama chini.
15Macho ya watu wote yakuelekea Wewe,
Nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16Waufumbua mkono wako,
Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
17BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
18 BWANA yu karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminifu.
19 Atawafanyia wamchao matakwa yao,
Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
20 BWANA huwahifadhi wote wampendao,
Na wote wasio haki atawaangamiza.
21Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA;
Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu
milele na milele.


Ni vyema tukamwambia Mungu ya kwamba tunatambua wema na ukuu wake katika maisha yetu kila siku na kwamba tunamtegemea kwa kila jambo.

Nakuachia wimbo huu wa I will Bless You LORD By Hillsong

Be Blessed.
Bye.