Monday, June 2, 2014

Amri Kuu Ya Kwanza Ni Ipi?(2)


Bwana Yesu asifiwe!
Somo hili ni muendelezo wa somo lililopita.

4.Unatenga muda wako kuwa naye.
Mungu ni namba moja katika maisha yetu.Tunapaswa kumpa haki yake ya kuwa namba moja katika kila eneo.Kuanzia tunapoamka asubuhi,cha kwanza ni kutulia na kumshukuru Mungu kwa fadhili,wema,ulinzi n.k juu ya maisha yetu katika kila eneo.Tunapaswa kumsikiliza pia na yeye anazungumza nini nasi,na kutii haraka kwa kutenda vile anavyotuamuru.Utii ni bora kuliko dhabihu 1Samweli 15:22

Mungu ni BaBa mwenye upendo wa hali ya juu.Tunapaswa kutenga muda wa kuzungumza naye na kumsikiliza.Muongozo wote,mafanikio mazuri na baraka zinazodumu hutokana na kusikiliza na kutii vyema sauti ya Mungu



5.Unatumia nguvu zako kushirikiana naye
Mungu ni roho.Ili kufanikisha kazi zake humu ulimwenguni,anahitaji mwili wa kushirikiana naye.Ndio maana Mungu akifanya makao ndani ya mtu,yule mtu anakuwa na uwezo ajabu.Ni Mungu anayetufanya kupitia mtu.

Mungu anahitaji sana usharika nasi na anapenda sana mtu anayeshirikiana naye,anayemtumikia,tena ANAMHESHIMU mtu huyo.Yohana 12:26 ' Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu'.

Ni ajabu jinsi gani kuheshimiwa na Mungu?Yaani Mkuu aliyekuumba anakuheshimu!Hata ukija mbele zake na hoja yoyote iliyondani ya mapenzi yake unawekwa 'first track' na inafanyika kama unavyotaka.Mungu ni mwema sana.



Kuna faida nyingi sana za Kumpenda Mungu na Kumfanya YEYE kuwa namba moja katika maisha yetu.
Inatupasa kukua na kuongezeka katika kumpenda Mungu

Kuna semina ambayo imeanza leo inayohusu mada hii ambayo imeandaliwa na Mwalimu wetu Mzuri kama tunavyomfahamu,Mwl.Mgisa Mtebe.

Somo: NGUVU YA UPENDO
           Faida na Nguvu zilizopo Katika Kukua na Kuongezeka Katika Kumpenda Mungu.

Mahali: Msasani Lutheran

Muda: 5pm-7pm

Nakuachia wimbo huu wa kumwambia Mungu jinsi tunavyompenda

  'As We Gather May Your Spirit work within Us ' By Maranatha


      Mpaka wakati ujao,

TANZANIA KWA YESU!

No comments:

Post a Comment