Tuesday, June 24, 2014

KUPOKEA UPONYAJI TOKA KWA MUNGU


Zaburi 103:1-4

1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.
2 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.
3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,
4 Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,

Kila Mwana wa Mungu ni lazima apokee uponyaji maana ni haki yake.Huwezi kumtumikia Mungu ipasavyo ukiwa katika hali ya ugonjwa.Mungu hufanya uponyaji wa Roho na Mwili kwa wana wake.

Isaya 53:4-5
4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 




Chanzo Cha Udhaifu na Magonjwa Ni Nini?

1. Dhambi
Warumi 5:12-19
Mtu anapoishi katika dhambi anakosa haki ya kuzuia magonjwa hivyo yanamtesa.Hii pia tunaiona katika kitabu cha Marko 2:5.Bwana Yesu alimwambia yule mwenye kupooza kwamba asitende dhambi tena.Magonjwa mengi ya kurithi hutokana na dhambi za wazazi,mababu,kizazi cha nyuma na mara nyingi huambatana na laana.Soma Katika kitabu cha Kutoka 20:1-5 tunaona Mungu hupatiliza kizazi hadi kizazi mpaka kizazi cha nne.

Unapomkiri Bwana Yesu na kumkaribisha katika maisha yako yote ya kale yanapita na kila kitu kinakuwa upya.Unakua uzao wa kiteule,kuhani wa kifalme maana unakuwa umezaliwa kwa roho si kwa mapenzi ya mwili tena.

Pia,Tafuta sana kujua maana ya jina lako na jina la ukoo wako maana kuna siri katika majina.Kama ni baya na huwezi kulibadilisha,kataa laana zinazoambatana nalo.



2.Mapepo
Marko 9:17-18
Luka 13:11
Unafahamu kuwa mauti na uzima vi katika ulimi wako Mithali 18:21
Shetani kwa kufahamu kwamba dhambi tuko macho nazo ameamua kutumia ukiri weut kuufanya uwe dhaifu.Pamoja na kujisikia udhaifu ukishaomba amini kwamba umeshapona.Nawe utakuwa mzima.Shetani ana tabia ya kutuweka katika uhalisia zaidi ya imani.Atakwambia bado kichwa si unasikia kinauma?Na ukisikiliza utasikia kinagonga kweli.Lakini jua hizo ni mbinu zake tu.Ukishaomba,amini umepona.Utakuja kushangaa kiliacha kuuma saa ngapi maana utajikuta mzima tu.Ndio maana Bwana Yesu alikuwa akiponya anawaambia kabisa,Imani yako imekuponya.

Ni kwa jinsi gani tunaweza kupokea uponyaji?
1.Ni lazima kufanywa upya nia zetu.
Tuache dhambi na kuishi maisha matakatifu.Maisha yetu yafananie na wokovu kwelikweli.Warumi  12:1-2

2. Kuwa na imani isiyo na mashaka
Soma Neno la Mungu na ujinene mwenyewe maandiko kulingana na hali unayoipitia.Kama ni magonjwa zungumza nayo bila kuangalia uhalisia.Jinenee maandiko yanayokutamkia uzima na afya na uamini.Kumbuka pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.Tumia imani yako kusimamia watu wa nyumbani mwako pia especially watoto wako wadogo ambao hawajajua kujisimamia na utamwona Mungu akiwa upande wako siku zote.



Mungu akubariki.

Nakuachia wimbo wa Heal me O LORD, By Don Moen



Mpaka wakati ujao...
TANZANIA KWA YESU!

No comments:

Post a Comment