Praise The Lord!
Unapokuwa ndani ya Yesu,unapaswa kujua haki zako.Kuzifahamu haki zako vyema,ni lazima usome Biblia,utafakari maandiko.Roho Mtakatifu atakukukumbusha na utaweza kutumia maandiko hayo pindi unapopatwa na hali fulani.
Mungu wetu,ni Mungu asiyeshindwa na jambo lolote.Anafanya kila kitu,na ni Mungu anayeponya.Ngoja nikupe ushuhuda kidogo...
Kati ya wanangu Mungu alionibarikia,nina mapacha.Sasa huyu pacha mdogo au kwa lugha nyingine dotto,alikuwa mzima tu lakini juzi jioni,alikuwa 'restless'.Analala kidogo,anaamka akiwa analia,na mara nyingine anashika kichwa huku analia.Hajajua kujielezea sana hivyo nilikuwa kwenye wakati mgumu kidogo kujua nini kinamsumbua.Kufika mida ya saa tatu usiku,alikuwa na dalili za joto,kula hajisikii yani hata vile vyakula anavyopenda sana nikimpa anavisogezea mbali.Nikajua kuna tatizo.Iwe malaria,iwe UTI, au nini lakini kuna tatizo.Nikamwambia Mungu pesa ulizonibarikia umeziwekea ulinzi tayari na kwamba utamkemea yule alaye isivyo halali maana mimi ni mtoto wako na ninatoa fungu la 10 sadaka na zaka.
Malaki 3:10-11 inasema
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.
(Hivi unafahamu kuwa kutokutoa fungu la 10,sadaka na zaka kunafanya kinyume cha hayo yaliyoandikwa hapo?Laana,mikosi,mabalaa yanapata milango hapo.Hili somo nitakuja kulifundisha muda si mrefu.It's very serious.It affects your spiritual and physical life indeed)
Nikamchukua mwanangu nikaingia naye chumbani,nikafungua Biblia,hatukwenda mbali tukaanza na Kumbukumbu la Torati 28:7
7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Nikamshikisha kwa mikono biblia huku nikimtakia maneno ya mstari huo.Baada ya hapo tukahamia kwenye Isaya 53:5
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Nikaanza kumwomba Mungu huku nikikemea kila hila za yule adui na kuachilia uzima na afya njema.Nilipomaliza,na yeye akajibu Amen.
Usiku wakati amelala nikaenda kumwangalia,nikakuta jasho linamtiririka sana,nikamfuta,nikamshukuru Mungu kwa uponyaji unaoendelea nikarudi kulala.Asubuhi alivyoamka tu akanifuata na kikombe akaniambia anataka maji ya kunywa.Nikampa.Baada ya hapo alikuwa anakula kila kitu,anakimbia,anacheza, kachangamka mnoo.Nilimshukuru Mungu kwa uponyaji huo.Mpaka sasa navyoandika hapa ni mzima kabisa.Yes,Mungu wetu ana nguvu,ni mkuu,hakuna neno gumu kwake.
,
Bwana Yesu alipokuwa anaponya watu,aliangalia pia kama wanaamini anaweza kuponya.
Soma Luka 17:19, Marko 10:52, Luka 8:48
Wale wote waliokuja kwake wakiwa wanaamini bila shaka kwamba atawaponya,walipona hapo hapo.
Licha ya mambo niliyoeleza hapo juu,imani yako pia inahusika sana.Kama unamwendea Mungu ukiwa una mashaka,umelikuza tatizo na kuliona ni kubwa kuliko Mungu wetu,hutaweza kupokea.Fanya upande wako ili na Mungu afanye upande wake.Mkabidhi Bwana Yesu maisha yako kwanza,muamini jumla,halafu ishi sawa sawa na Neno Lake.
Mpaka wakati ujao..
TANZANIA KWA YESU!

No comments:
Post a Comment