Thursday, July 17, 2014

UAMINIFU WA MUNGU NI MKUU





Kumbukumbu 7:9

9 Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu;

Praise The LORD!
Mungu wetu ni mwaminifu mnoo!Haijalishi umemwomba nini ali mradi iwe sawasawa na mapenzi yake na uwe unamcha na kumpenda,atafanya.Unapomwomba,muamini.Muachie.
Isaya 41:21 amesema "Haya,leteni maneno yenu,asema BWANA;toeni hoja zenu zenye nguvu,asema mfalme wa Yakobo'.



Ukiona ka-muda kanakwenda,mkumbushe.Maana amesema hata kwenye neno lake katika Isaya 43:26 'Unikumbushe,na tuhojiane;eleza mambo yako,upate kupewa haki yako.'

Nina ushuhuda wa haraka ambao umenitokea leo hii hii juu ya jambo hili.Wiki mbili zilizopita kuna jambo fulani ambalo nilikuwa ninalihitaji mno mno kulifanya na ufumbuzi wake usipite hizi wiki mbili.Nilipokuwa naomba usiku nikamshirikisha Mungu.Wakati naendelea kuomba nikasikia sauti ya utulivu sana ikiniambia mshirikishe 'fulani' hilo jambo.Pale pale nikajua Mungu anataka kumtumia huyo mtu kunisaidia kulipatia ufumbuzi.Nikamwomba palepale Mungu kibali kwamba nitakapoenda kumshirikisha huyo mtu,alipokee,na anipatie ufumbuzi.Hiyo ilikuwa ni wiki mbili zilizopita.

Kesho yake nikampigia simu yule mtu,tukaongea vizuri akaniambia jioni ya siku inayofuata tuonane.Siku iliyofuatia kweli nikaenda.Nikamshirikisha kila kitu lakini cha kushangaza nilisahau kumwambia deadline.Akaniambia nimuachie alifanyie kazi.Tukaachana.Kwa kifupi alikuwa ameelewa.Wiki ikapita,huku naona wiki moja tu imebaki linatakiwa ufumbuzi.Nikampigia simu yule mtu kumkumbusha,akanipa jibu la nusu nusu au fifty fifty.Ni kama atanisaidia lakini inavyoonekana itakuwa nje ya muda ambao jambo hili linahitaji.Kwa maana nyingine hata akinisaidia muda huo kama ni zaidi ya wiki moja ambayo ndiyo imebaki,huo msaada hautakuwa na maana tena kwangu maana muda utakuwa umepita.Nikawa mpole.



Mwisho wa hiyo siku ulikuwa ni kesho.Toka jana jioni nilikuwa katika hali ya upole sana.Shetani naye hakucheza mbali  nilikuwa nasikia enhe?! za hapa na pale.'Enhe?!kiko wapi?Yuko wapi Mungu?au ndo ushaharibu mahali.Mbona hajibu.Utakuwa umeharibu mbona hajibu?Nilimwambia shetani hata uongee vipi hainibadilishi kutokuwa mtoto wa Mungu na nikamwambia Mungu hata kama halitafanyika utabaki kuwa Mungu,hautabadilika,wala mtazamo wangu kwako hautabadilika.Hayo ndiyo maneno niliyokuwa nayasema kila nikikumbuka kwamba muda unakwisha halafu kimyaa!

Leo asubuhi nikaamka nikamshukuru Mungu kwa kifupi tu,nikasema maneno yale yale tena utabaki kuwa Mungu kwangu na nitakuabudu siku zote mimi na familia yangu.Ikafika kama saa tano asubuhi,nikakaa chini mahali nikamwambia Mungu nakutegemea,naomba unisaidie.Nikaondoka kwenda na mambo yangu mengine.Nilipofika napokwenda nilipotulia chini nikaona missed call ya yule mtu ilipigwa kumbe saa sita kasoro nadhani nikiwa naendesha  gari, simu ipo kwenye pochi sikusikia.Nikampigia yule mtu,akaniambia nimekutafuta kwenye simu sana,nimeshalipatia ufumbuzi jambo lako uje leo hii hii!Yani alikuwa anaongea kwa msisitizo kama vile nisikose.Haleluya!Mimi nimeshangaa kwa sababu yule mtu hakuwa anajua 'deadline' ya hilo jambo kuwa ni kesho.
Huyu ndiye MUNGU tunayemwabudu aisee.Nina shuhuda nyingi mno mno kwenye maisha yangu katika nyakati tofauti ambazo Mungu amekuwa akinitendea mambo makuu.Tutakuwa tunashirikishana.



Zaburi 91:4
4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

Kwa leo naishia hapa.Mungu akubariki.


No comments:

Post a Comment