Friday, August 15, 2014

Namna Kumi na moja(11) Za Kumpendeza Mungu


Praise The LORD!

Wengi wetu tunatamani kumpendeza Mungu.Unapokuwa unampenda mtu fulani ni dhahiri kwamba hupendi kumuudhi na mara nyingi utataka kujua ni vitu gani anafurahishwa navyo ili uvifanye azidi kukufurahia.Kwa Mungu naye ni hivyo hivyo.Kuna mambo kadhaa ambayo unaweza kuyafanya ukamfurahisha sana Mungu.Mimi nimefanikiwa kukuletea mambo kumi na moja(11) kutoka kwenye maandiko,ambayo unaweza kuyafanya ukampendeza Mungu.

1.KUMWAMINI MUNGU- Waebrania 11:6
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.



2.KUMSIFU BWANA NA KUMTAFAKARI KWA FURAHA KILA WAKATI-Zaburi 104:33-34
33 Nitamwimbia Bwana maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai;
34 Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Mimi nitamfurahia Bwana.
Biblia ya kiingereza imeandika vizuri badala ya Neno 'na kuwe kutamu kwake' imetumia neno 'pleasing' kama ifuatavyo:
33 I will sing to the LORD all my life; I will sing praise to my God as long as I live.
34 May my meditation be pleasing to Him, as I rejoice in the LORD.

3.KUJITOA KWA MUNGU-Warumi 12:1
1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

4.KUOMBEA DUNIA NA MAMLAKA ZILIZOPO -1 Tim. 2:1-3

1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;

 Biblia ya kiingereza imetumia neno pleases katika mstari wa tatu badala ya neno 'lakubalika',kama ifuatavyo....

I urge, then, first of all, that requests, prayers, intercession and thanksgiving be made for everyone - for kings and all those in authority, that we may live peaceful and quiet lives in all godliness and holiness. This is good, and pleases God our Saviour.



5.KUZAA MATUNDA NA 
6.KUMFAHAMU MUNGU ZAIDI - Wakolosai 1:10
mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;

7. KUZIPA KIPAUMBELE AFYA ZA KIROHO ZA WAKRISTO WENGINE -Warumi 14:15-18
15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.
17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
18 Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.



8. KUWATENDEA SAWA WA NYUMBANI MWAKO -Wakolosai 3:18-21,1Timotheo 5:4
Wakolosai 3:18-21
18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.
19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
20 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.
21 Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

9.UTOAJI -Wafilipi 4:18
18 Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.

10.KUFANYA HAKI KWENYE BIASHARA ZAKO -Mithali 11:1
1 Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.

11.KUENENDA KATIKA MAPENZI YA MUNGU -1Wasethalonike 4:1
1 Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.




Nakuachia wimbo huu Umpendeze nao Bwana, wa Lord I lift you name on High



Mpaka wakati ujao,
TANZANIA KWA YESU!

Tuesday, August 12, 2014

Today's Prayer...




Jipe Moyo Mkuu,Jikabidhi Kwa BWANA.

ZABURI 27

1 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
2 Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
3 Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.
4 Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.
5 Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.
6 Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi Bwana.
7 Ee Bwana, usikie, kwa sauti yangu ninalia, Unifadhili, unijibu.
8 Uliposema, Nitafuteni uso wangu, Moyo wangu umekuambia, Bwana, uso wako nitautafuta.
9 Usinifiche uso wako, Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira. Umekuwa msaada wangu, usinitupe, Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.
10 Baba yangu na mama yangu wameniacha, Bali Bwana atanikaribisha kwake.
11 Ee Bwana, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea;
12 Usinitie katika nia ya watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo wameniondokea, Nao watoao jeuri kama pumzi.
13 Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana Katika nchi ya walio hai.
14 Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.



Usisahau kuwaombea na wengine 


Mpaka wakati ujao,

TANZANIA KWA YESU!

Wednesday, August 6, 2014

Imani Yako Imekuponya



Praise The Lord!

Unapokuwa ndani ya Yesu,unapaswa kujua haki zako.Kuzifahamu haki zako vyema,ni lazima usome Biblia,utafakari maandiko.Roho Mtakatifu atakukukumbusha na utaweza kutumia maandiko hayo pindi unapopatwa na hali fulani.

Mungu wetu,ni Mungu asiyeshindwa na jambo lolote.Anafanya kila kitu,na ni Mungu anayeponya.Ngoja nikupe ushuhuda kidogo...



Kati ya wanangu Mungu alionibarikia,nina mapacha.Sasa huyu pacha mdogo au kwa lugha nyingine dotto,alikuwa mzima tu lakini juzi jioni,alikuwa 'restless'.Analala kidogo,anaamka akiwa analia,na mara nyingine anashika kichwa huku analia.Hajajua kujielezea sana hivyo nilikuwa kwenye wakati mgumu kidogo kujua nini kinamsumbua.Kufika mida ya saa tatu usiku,alikuwa na dalili za joto,kula hajisikii yani hata vile vyakula anavyopenda sana nikimpa anavisogezea mbali.Nikajua kuna tatizo.Iwe malaria,iwe UTI, au nini lakini kuna tatizo.Nikamwambia Mungu pesa ulizonibarikia umeziwekea ulinzi tayari na kwamba utamkemea yule alaye isivyo halali maana mimi ni mtoto wako na ninatoa fungu la 10 sadaka na zaka.

Malaki 3:10-11 inasema
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.

(Hivi unafahamu kuwa kutokutoa fungu la 10,sadaka na zaka kunafanya kinyume cha hayo yaliyoandikwa hapo?Laana,mikosi,mabalaa yanapata milango hapo.Hili somo nitakuja kulifundisha muda si mrefu.It's very serious.It affects your spiritual and physical life indeed)



Nikamchukua mwanangu nikaingia naye chumbani,nikafungua Biblia,hatukwenda mbali tukaanza na Kumbukumbu la Torati 28:7
7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Nikamshikisha kwa mikono biblia huku nikimtakia maneno ya mstari huo.Baada ya hapo tukahamia kwenye Isaya 53:5
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.


Nikaanza kumwomba Mungu huku nikikemea kila hila za yule adui na kuachilia uzima na afya njema.Nilipomaliza,na yeye akajibu Amen.
Usiku wakati amelala nikaenda kumwangalia,nikakuta jasho linamtiririka sana,nikamfuta,nikamshukuru Mungu kwa uponyaji unaoendelea nikarudi kulala.Asubuhi alivyoamka tu akanifuata na kikombe akaniambia anataka maji ya kunywa.Nikampa.Baada ya hapo alikuwa anakula kila kitu,anakimbia,anacheza, kachangamka mnoo.Nilimshukuru Mungu kwa uponyaji huo.Mpaka sasa navyoandika hapa ni mzima kabisa.Yes,Mungu wetu ana nguvu,ni mkuu,hakuna neno gumu kwake.
,
Bwana Yesu alipokuwa anaponya watu,aliangalia pia kama wanaamini anaweza kuponya.
Soma Luka 17:19, Marko 10:52, Luka 8:48
Wale wote waliokuja kwake wakiwa wanaamini bila shaka kwamba atawaponya,walipona hapo hapo.
Licha ya mambo niliyoeleza hapo juu,imani yako pia inahusika sana.Kama unamwendea Mungu ukiwa una mashaka,umelikuza tatizo na kuliona ni kubwa kuliko Mungu wetu,hutaweza kupokea.Fanya upande wako ili na Mungu afanye upande wake.Mkabidhi Bwana Yesu maisha yako kwanza,muamini jumla,halafu ishi sawa sawa na Neno Lake.



Mpaka wakati ujao..
TANZANIA KWA YESU!

Saturday, August 2, 2014

Moyo Wa Shukrani Huku Ukimtarajia BWANA



Praise The LORD!

Kila mmoja wetu chini ya jua ameshakuwa na hitaji la namna fulani ambalo alishawahi kutulia na kumwomba Mungu,akajibu.Unapoomba unatakiwa kuamini na kinachofuata tunatakiwa kushukuru.Ukikaa chini ukitafakari vizuri utagundua Mungu alijibu maombi yako mara kadhaa kwenye maisha yako,kama si yote.Je, huwa tunarudi mbele zake kwa ajili ya kumshukuru?

Kuna maombi mengine,ambayo yanahitaji usubiri majibu.Hata unapotuma maombi yoyote,iwe ya kazi au yoyote,itakupasa usubiri majibu.Inaweza ikawa masaa kadhaa,miezi kadhaa au miaka kadhaa.


                          Hold on,HE is going to turn green lights on,sooner than you think.


Kumshukuru Mungu kabla hata jambo halijaonekana dhahiri kwa macho kunaonyesha ni kiasi gani unamwamini kwamba atafanya.Inawezekana ukaona umeishiwa maneno ya kumwambia Bwana ambayo yatawakilisha shukrani zako kwake.Zaburi 138 ni msaada mkubwa katika kumshukuru Mungu ukiwa umtarajia kwamba atafanya.

Zaburi 138

1 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote.
3 Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
4 Ee Bwana, wafalme wote wa dunia watakushukuru, Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.
5 Naam, wataziimba njia za Bwana, Kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.
6 Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.
7 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa kuume utaniokoa.
8 Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.

Anapokuja kujibu maombi yako,ni vyema ukafanya kama ulivyomuahidi,ya kwamba utamshukuru kwa moyo wako wote,utasujudu ukilikabili hekalu lake takatifu..n.k



Mungu ni mwaminifu mno.Unapoomba sawasawa na mapenzi yake hujibu.

Mpaka wakati ujao...
TANZANIA KWA YESU!