Friday, June 13, 2014

Mambo Saba (7) Ya Kufanya Unapopatwa Na Uoga -2


Blessed Be The Name Of The LORD, Halelujah!
Somo letu linaendelea....

(4)Amini Nguvu Za Mungu
Zaburi 27:1-3
1 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
2 Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
3 Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.



Na lingine hili....
Isaya 41:10
10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Hivi umegundua ulivyokuwa mtoto maisha yalikuwa hayakutishi kihivyo?Ulikuwa huna woga wala wasiwasi na chochote kile.Tena mtu akikubugudhi unamwambia nitakusemea kwa baba/mama akirudi.Unakumbuka?
Unatakiwa kuishi kwa staili hiyohiyo,bila woga wala wasiwasi na ukibughudhi nenda msemee kwa Baba Wa Mbinguni maana kwanza ni haki na urithi wako kulindwa na kutetewa na Baba wa Mbinguni Isaya 54:17

(5)Woga hautokani na Mungu
2Timotheo 1:7
7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Woga hautokani na Mungu.Angalia chanzo cha woga wako na katika kufikiri utagundua kwamba hatumwamini Mungu vizuri kwamba anaweza kudhibiti hali tunayopitia ndio maana tunaogopa.Mungu anataka tumwamini asilimia mia.Ni Baba mwenye upendo,atakutetea.



(6)Ni Mungu Anayejali
1Petro 6:6,7
6 Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;
7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Hivi ungejisikiaje kama mtoto wako anakuja anakwambia changamoto anazopitia  halafu unamwambia niachie mimi nitashughulikia,halafu anaondoka anaendelea kupambana na changamoto hiyo katika kiwango cha kushindwa anafanya ndivyo sivyo si inasikitisha sana?Ndivyo ilivyo kwa Baba yetu wa Mbinguni.Anataka tumtwishe yeye fadhaa zetu.Maana anajishughulisha sana na mambo yetu 1Petro 5:7




Nakuachia wimbo wa 'He Knows My Name' By Israel & New Breeds
 Mungu anakufahamu kwa Jina.Anafahamu mwisho wako kabla hata hajakuumba.Stop worrying and cast your cares upon Him.He will never fail you.




Mpaka wakati ujao.....
TANZANIA KWA YESU!
 


No comments:

Post a Comment