Thursday, June 19, 2014

Tengeneza Msingi Wa Maisha Ya Kiroho Kwa Watoto Wako




Mithali 22:6
6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Malezi ya watoto huanza toka angali tumboni.Ni vizuri wazazi tukawa na muda wa kuzungumza vizuri kwa upendo na watoto wetu angali wako tumboni.Hiyo peke yake inajenga upendo wa pekee baina ya mtoto na wazazi wake.Anapozaliwa,kuanzia hapo ndipo unapaswa kuongeza nguvu ya ziada katika kumlea.

Kumfundisha kuenenda katika njia inayompasa ni Jukumu letu wazazi na ni Haki ya mtoto wako.Namna atakavyokuwa ukubwani ni matokeo ya malezi yake ya utotoni.Ukimuongoza vyema kuanzia mapema atakuwa mtu mzuri na mwema baadaye kadhalika kwa upande wa pili wa kumuongoza vibaya.



Mungu ametupa jukumu la kulea wanetu kwa kipindi kifupi sana.Baada ya hapo Mungu huwafundisha mwenyewe huku akiwapa amani nyingi sana kwenye maisha yao.Isaya 54:13
13 Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.

Kazi yako ni kuwajengea msingi wanetu huku tukimshirikisha Bwana. Mithali 22:6.
Hiyo njia tunayopaswa kulea wanetu ni ipi?Tuangalie Matayo 7:13-14
13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.



Njia ya kwenda uzimani waionao ni wachache sana.

Njia ya kwenda uzimani ni ipi? Yohana 14:6
 'Mimi ndimi njia,na kweli na uzima.Mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi.'
Hayo ni maneno ya Bwana Yesu mwenyewe.Mtu hawezi kwenda mbinguni ila kwa njia ya kumkubali Yesu.Ndio ukweli wenyewe, maandiko yako wazi.Ukiliona hili wewe ni kati ya wachache waliotamkwa kwamba wanaiona.
Mimi nimechagua njia ya kwenda uzimani na Namwomba Mungu wanangu wakae katika njia hiyo hiyo ya kwenda uzimani.Wewe ungependa mwanao/wanao wakae njia ipi?

Mathayo 22:37
37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
Wafundishe wanao kumpenda Mungu JUMLA.Mungu ni mwingi wa rehema,huruma na fadhili kwa wale wampendao.

Kumbukumbu la Torati 5:6-10
6 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
7 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
8 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi.
9 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
10 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.




Endapo hujafanya maamuzi,fanya maamuzi sahihi sasa.Ingia katika njia iendayo uzimani ili ufanikiwe kuwaingiza watoto wako katika njia iendayo uzimani pia.Mkubali Bwana Yesu abadilishe maisha yako.

Mungu akubariki.Mpaka wakati ujao...

TANZANIA KWA YESU!


No comments:

Post a Comment