Zaburi 95 , 96 , 100
Praise The Lord!
Leo nimeamka nikatulizana hapohapo kitandani kimya nikamtafakari Mungu.Nikaanza ku-analyse jinsi anavyoshughulika na maisha yangu,familia yangu,jinsi anavyoshughulika na kazi zangu,biashara zangu,watu walio karibu yangu,kwa kweli moyo wangu uliishia kumshukuru kwa machozi ya furaha.
Mungu ni mwema sana.Anajishughulisha mno na maisha yetu.Amejaa upendo juu yetu na anahurumia sana wanaomcha YeYe.(Zaburi)
Tuna kila sababu ya kumshukuru sana Mungu.Uzima/Uhai,nguvu,Furaha,Amani,afya njema na mengineyo ni sababu tosha ya kumshukuru Mungu.Mimi nimemuona binafsi akishughulika na maisha yangu kila siku.Kila jambo ninalotaka kufanya huwa namshirikisha,nikipata amani kutoka kwenye kina cha moyo nalifanya.'Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo ninyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!(Wakolosai 3:15)
Shukrani ni sehemu ya maombi.'Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; '(1Timotheo 2:1). Ni vyema ukatanguliza shukrani zako mbele za Baba,mwambie jinsi unatambua uwepo wake na msaada wake katika maisha yako,mwambie jinsi alivyo mkuu n.k.Yeye ni Mungu,Muumba wa Mbingu na nchi,na vyote, na itabaki kuwa hivyo, hiyo tu ni sababu tosha ya kumshukuru achilia mbali mengine aliyotubariki.Anastahili.
Kumshukuru Mungu ni muhimu nyakati zote maana kuna nyakati chini ya jua Mhubiri 3:1-8. Unapokuwa mtu wa shukrani,moyo wa Mungu unafurahi.Hata kama ni wewe una mwanao mmoja huyo yeye ukimpa pipi anakushukuru kama vile umempa gari,na ukimpa gari anakushukuru vizuri sana kwa kiwango hicho hicho nadhani ungempenda sana tofauti na yule ambaye ukimpa pipi hashukuru.Huyo ana dalili hata ukimpa gari ataona ni kawaida tu.Hatashukuru.'Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. '(Mathayo 25:29)
Hata ndege asubuhi huamka na nyimbo za furaha na shukrani.Kumbuka sana kumshukuru Mungu kila unapoamka na kabla ya kulala.Hata kwa maneno machache tu,kama umechoka sana.Baba yetu ni muelewa mno.
Nitaendelea...Nakuacha na wimbo 'When I think of You' by Michael W Smith.
Oh! napenda hiyo chorus yake..Yahweh!There is no one like You Lord
Yahweh! Halelujah, we sing,
Yahweh!There is no one like You Lord
Yahweh!Your banner for me,Your banner for me,is LOVE!
Mpaka wakati ujao,
TANZANIA KWA YESU!
No comments:
Post a Comment