Hapa tunaona makusudi ya Bwana Yesu kuja ulimwenguni.Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu(Warumi 3:23) na mshahara wa dhambi ni mauti(Warumi 6:23) hivyo kwa kuwa Mungu anatupenda sana hakutaka tuangamie bali tuwe na uzima wa milele (Yohana 3:16)
Unachotakiwa kufanya ni kumkiri Yesu kwa kinywa chako na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu,utaokoka.(Warumi 10:9)
Bila kufanya hili hutaweza kukanyaga kamwe Ufalme Wa Mungu.Dini haimpeleki mtu mbinguni hata Yesu aliulizwa na wanafunzi wake dini safi ni ipi akajibu nini?Alizungumzia matendo mema kama kuwaona wagonjwa,kusaidia yatima,wajane n.k..lakini hapo hapo kufanya hayo yote hayatoshi kama hutamkiri Yesu kuwa Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka wafu.Tuangalie uhalisia.Kuna watu wangapi unapishana nao huko barabarani tena wako vizuri tu.Lakini kwa sababu huna mahusiano nao,huwafahamu,huwezi kuwakaribisha nyumbani mwako.Lakini katika kupita kwako ukakutana na rafiki yako ambaye mna mahusiano mazuri utamkaribisha kwako.Hata Yesu ni hivyo hivyo.
Kama bado hujampokea Yesu,fuatisha sala hii ili utengeneze mahusiano yako na Mungu.
"Bwana Yesu,nipo mbele zako,ninatubu dhambi zangu.Naomba unisamehe,unisafishe kwa damu yako ya thamani.Ninaamini ulikufa msalabani kwa ajili yangu na siku ya tatu ukafufuka,ukapaa mbinguni.Naomba ulifute jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima.Ninaahidi kuambatana nawe kuanzia sasa katika maisha yangu yote.Amen."
Hongera kwa kumpokea Bwana Yesu na Karibu sana katika familia ya Yesu.
Naomba utafute kanisa zuri lenye misingi ya Biblia litakolokusaidia kukua kiroho.Mungu akubariki.
Tukutane wakati ujao tena...Mungu akubariki..
No comments:
Post a Comment